Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 19:24

UN: Afrika yapoteza mabilioni ya dola kwa fedha haramu kila mwaka


Makao makuuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani
Makao makuuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani

Utafiti uliondeshwa na Umoja wa Mataifa, umeonyesha bara la Afrika linapoteza karibu dola billioni 89 kila mwaka katika mtiririko haramu fedha kama vile ukwepaji kodi na wizi.

Ripoti hiyo yenye kurasa 248, iliyotolewa Jumatatu, imetolewa na bodi ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD.

Ripoti inaeleza fedha zinazopotea ni zaidi ya zile ambazo bara la Afrika inazipata katika misaada ya maendeleo, na makadirio hayo ni makubwa zaidi kuliko ya awali.

“Mtiririko haramu wa kifedha unaibia Afrika, na kufifisha matarajio ya watu wake, unadhoofisha uwazi, na uwajibikaji na kuharibu imani kwa taasisi za kiafrika," amesema katibu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi.

Karibu nusu ya hasara ya dola billioni 88.6 kwa mwaka ni mapato ya bidhaa zinazouzwa nje kama vile dhahabu, almasi na madini ya platinum, kwa mujibu wa ripoti ya UNCTAD.

XS
SM
MD
LG