Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:58

Afrika yaelezwa kuwa na kazi kubwa kushughulikia haki za binadamu


Shirika la kutetea  haki za binadamu la Human Rights Watch, limesema  nchi za Afrika zina kazi kubwa ya kufanya, ili kushughulikia matatizo yaliyosambaa ya ukosefu wa makazi,  mauaji,  na  ukiukaji mwingine unaotokana na migogoro mingi barani humo.

Kundi la kutetea haki limechapisha ripoti mpya wiki hii ambayo imetoa muhtasari wa matukio katika nchi 23 za Afrika.

Mausi Segun, mkuu wa Human Rights Watch kanda ya Afrika, amesema, watu wamejikuta kwenye mgogoro na hawajui pa kukimbilia.

Baadhi ya matukio mabaya ya ukiukaji wa haki za binadamu yanaendelea kutokea wakati wa vita” Segun amesema.

“Raia wanaendelea kubeba mzigo wa mashambulizi ya silaha, unyanyasaji ya kijamii, machafuko ya kisiasa na kijamii pamoja na ukandamizaji unaofanywa na serikali dhidi ya wakosoaji na sauti huru katika nchi kadhaa za kiafrika. Haya yote yamesababisha uharibifu wa maisha.

Kwa mujibu wa shirika la ACLED, the Armed Conflict Location na Event Data Project, kulikuwa na matukio yasiyopungua 36,000 ya unyanyasaji na zaidi ya vifo 50,000 vilivyosababishwa na vurugu barani Afrika mwaka wa jana.

Shirika la Human Rights Watch, limesema kuna takriban mizozo ya silaha 15, katika maeneo ya Sahel, bonde la Ziwa Chad, na eneo la Maziwa Makuu na huko katika Pembe ya Afrika. Majeshi ya serikali na makundi yenye silaha yamekuwa yakijihusisha na vitendo vya kikatili dhidi ya raia.

“Katika matukio mengi, waasi wenye silaha na majeshi ya serikali yamesabisha vitisho kwa raia ambao wamejikuta katikati ya mapigano” Segun amesema “na kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbilia maeneo mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya kitaifa ambako pia wanakabiliwa na hali ya ubaguzi, kutokukubalika, chuki na wakati mwingine kusababisha kukataliwa.

Ukosefu wa ustahmilivu wa kisiasa, kidini na kijamii pia imeongezeka, kwa mujibu wa watafiti ya haki za binadamu.

Ripoti imesema kauli za chuki, mashumbulizi dhidi ya wapinzani kisiasa, ongezeko la ushindani wa rasilimali and sababu nyingine zinaendelea kusababisha mivutano ya kijamii, uasi na uandikishaji wa vikundi venye misimamo mkali kwa baadhi ya nchi za Afrika

Kundi la kutetea haki limeipongeza Umoja wa Afrika na taasisi nyingine za kikanda ikiwemo ECOWAS kwa kuchukuahatua, kama vile usuluhishi wa mgogoro mkali wa Ethiopia, kulaani mapinduzi ya kijeshi Afrika Magharibi, na kukataa kutambua uchukuaji madaraka kinguvu.

Carine Kaneza Nantulya ni mkurugenzi msaidizi wa Human Rights Watch kitengo cha Afrika, amesema taasisi ya bara hilo haifanyi vya kutosha kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG