Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 18:09

Afrika yadumaa katika utowaji chanjo


Mwanamke mmasai akipokea chanjo ya Covid, kwenye zahanati kusini mwa Kenya Agasti 28, 2021
Mwanamke mmasai akipokea chanjo ya Covid, kwenye zahanati kusini mwa Kenya Agasti 28, 2021

Katika taarifa yake, WHO inaeleza kuwa ni asilimia 24 pekee ya wakazi wa bara hilo ambao wamepata chanjo kamili za Covid, ikilinganishwa na asilimia 64 katika maeneo mengine ya ulimwengu.
Liberia, Mauritius na Seychelles wamechanja takriban asilimia 70 ya raia wao.
Huduma za utoaji chanjo zinaonekana kwenda kasi ya pole pole kote barani humo katika miezi ya karibuni.
Maafisa wa afya wametoa takriban chanjo millioni 23 kote barani Afrika hapo mwezi Septemba,ikilinganishwa na chanjo takriban millioni 47 zilotolewa mwezi Julai.
Mkurugenzi WHO kwa kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti, ameeleza kuwa japo mlipuko wa Covid unaonekana kumalizika, lakini pia unaweza kurudi tena kwa nguvu, ikiwa Afrika bado inabakia nyuma katika kupata kinga kutokana na virusi hivyo.

XS
SM
MD
LG