Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 18:05

Rais wa Afrika ya Kati ataka waondolewe vikwazo vya silaha.


Rais Afrika ya kati Faustine Archange Touadera alipozungumza na VOA.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati anasema anataka umoja wa mataifa kundoa marufuku ya silaha kwenye nchi yake.

Katika mahojiano na VOA rais Faustine Archange Touadera alisema vikwazo vilivyowekwa 2013 vilikuwa vya haki kwa wakati ule lakini kwa sasa vimepitwa na wakati.

Kumefanyika uchaguzi, serikali halali imeundwa na pia bunge alieleza. Tunaweka taasisi za kidemokrasia na hatuwezi kuwa na jeshi bila silaha.

Touadera amesema anataka kulijenga upya jeshi. “nahitaji jeshi la kitaifa lenye weledi na linalowakilisha kila kabila ambalo watu wote wa Afrika ya kati watalitambua hii ndio dhamira yetu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG