Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:09

Afrika Kusini: Zuma amshtaki Ramaphosa kwa madai ya kuvujisha ripoti yake ya afya


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mjini Johannesburg, Oktoba 22, 2022. Picha ya AFP
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mjini Johannesburg, Oktoba 22, 2022. Picha ya AFP

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kwamba anamshtaki Rais Cyril Ramaphosa kutokana na ripoti ya afya iliyovuja inayohusiana na kesi ya rushwa ya silaha ya mwaka 1990.

Tangazo hilo ambalo limetolewa usiku wa kuamkia leo, linajiri wakati chama tawala cha African National Congress kikianza kongamano leo Ijumaa ambalo linatarajiwa kumchagua tena Ramaphosa kama kiongozi wa chama, ambaye mwenyewe anakabiliwa na kashfa kubwa ya pesa.

Zuma alitangaza kuwa ameanzisha mashtaka binafsi jana Alhamisi dhidi ya Ramaphosa, akimtuhumu kuwa alisaidia katika kuvujisha waraka wa siri wa matibabu kuhusu Zuma kwa vyombo vya habari.

Kesi hiyo inahusiana na kampeni ya muda mrefu ya Zuma lakini hadi sasa haikufanikiwa kumuondoa mwendesha mashtaka Billy Downer, ambaye anamfuatilia rais huyo wa zamani kwa tuhuma za rushwa zinazohusiana na mkataba wa ununuzi wa silaha mwaka 1990.

XS
SM
MD
LG