Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 21:18

Afrika kusini yathibitisha aina mbili za maambukizi ya virusi vya Corona


Picha inayoonyesha mfano wa virusi vya Corona
Picha inayoonyesha mfano wa virusi vya Corona

Maafisa kutoka taasisi ya kitaifa ya magonjwa ya kuambukiza nchini humo walitangaza Jumapili wamegundua aina mpya ya virusi B.1.617.2 na B.1.1.7 kwa watu wa Afrika kusini

Maafisa wa Afrika kusini wanasema aina mbili mpya za virusi vya Corona vinavyoambukiza, hivi sasa vipo nchini humo, wakati taifa hilo lililoathiriwa vibaya barani Afrika linajiandaa kwa uwezekano wa kuwa na kesi mpya.

Maafisa kutoka taasisi ya kitaifa ya magonjwa ya kuambukiza nchini humo walitangaza Jumapili kwamba wamegundua aina mpya ya virusi B.1.617.2 na B.1.1.7 kwa watu wa Afrika kusini.

Kukiwa na kesi chini ya milioni 1.6 zilizothibitishwa katika nchi hiyo ya Afrika kusini inayoongoza barani Afrika katika maambukizi ya virusi vya Corona. Kati ya kesi hizo, karibu watu 55,000 wamekufa.

Aina ya kwanza ya kirusi B.1.617.2 imegunduliwa katika kesi nne ambazo zilionyesha matokeo "positive" taasisi hiyo ilisema. Kesi mbili kati ya hizo zipo huko Gauteng, mkoa wenye idadi kubwa ya watu na ni makazi ya jiji la Johannesburg na Pretoria.

XS
SM
MD
LG