Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:24

Afrika kusini yataabika na umeme


Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa.

Kampuni hiyo ambayo inasambaza umeme kwa asilimia 90 nchini humo imetaabika kufikia uhitaji wa umeme Afrika kusini kwa muongo mmoja.

Mipango ya serikali kumaliza matukio ya mgao na kukatika umeme inaweza kukamilika angalau baada yam waka mmoja ili matokeo mazuri yaweze kuonekana , amesema hayo mkurugenzi wa juu wa Eskom .

Licha ya rais Cyril Ramaphosa kuahidi hatua mpya za kukabiliana na mzozo wa nishati nchini Afrika kusini lakini bado inaonekana kwamba taifa hilo lenye viwanda vingi litaendelea kukabiliwa na tatizo la umeme kwa takriban mwaka mmoja.

Kampuni hiyo ya serikali ya Eskom imekata umeme kwa kiasi kikubwa wiki iliyopita na inatarajiwa kufanya hivyo tena wiki hii. Mkurugenzi mkuu wa maswala ya operesheni wa ESKOM Bwana Jan Oberholzer alisema kuna mipango mingi inayotakiwa kufanyiwa kazi, ingawa itachukua muda kuitekeleza.

Amesema hadi sasa Eskom imetumia dola milioni 451 kwa ajili ya mafuta ya Diesel kwa ajili kufanya operesheni za genereta hiyo ni zaidi ya bajeti iliyokuwepo hali inayozua wasiwasi mkubwa.

XS
SM
MD
LG