Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:31

Afrika Kusini yasaidia Swaziland


Waandamanaji wa Swaziland wanaotaka mabadiliko ya kiutawala nchini mwao

Afrika Kusini yatoa zaidi ya dola milioni 350 kuikwamua Swaziland

Makundi ya Upinzani nchini Swaziland yameshtumu vikali uamuzi wa Afrika Kusini wa kutoa fedha kuikwamua serikali yao ambayo bado inatawaliwa na familia ya kifalme. Jumatano Afrika Kusini ilitangaza msaada wa zaidi dola ya milioni 350 kuisaidia nchi jirani ambayo imepungukiwa na fedha. Fedha hizo zinalenga kumsaidia mfalme Mswati kufanya mageuzi ya kiuchumi na kisiasa. Lakini wapinzani wa Swaziland wanasema Afrika Kusini ilipaswa kushinikiza mabadiliko ya kisiasa na kichumi yatekelezwe mara moja. Vyama vya upinzani ni marufuku nchini Swaziland na wanaharakati wengi wanamshtumu mfalme Mswati kwa ufisadi na pia kuvuruga uchumi.Taifa hilo la kusini mwa Afrika linakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha na limekumbwa na wimbi la maandamano tangu mwezi Aprili huku raia wengi wakitaka kuwe na mfumo wa utawala wa kidemokrasia. Mnamo mwezi Juni waziri wa fedha wa Swaziland Majozi Sithole alisema mishahara ya wafanyikazi wa serikali huenda ikacheleweshwa au kupunguzwa kwa nusu katika miezi ijayo, ikiwa taifa hilo halitapata mikopo.

XS
SM
MD
LG