Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:59

Afrika Kusini: Watu 4 wauawa katika maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za umeme


Wakazi waonekana wakipita karibu na nguzo za umeme wakati umeme wa kampuni ya Eskom ukikatika mara kwa mara, Aprili 4, 2022. Picha ya Reuters
Wakazi waonekana wakipita karibu na nguzo za umeme wakati umeme wa kampuni ya Eskom ukikatika mara kwa mara, Aprili 4, 2022. Picha ya Reuters

Watu wanne waliuawa Jumatatu wakati wa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za umeme katika kitongoji kimoja nchini humo, maafisa wamesema.

Wakazi wenye hasira kutokana na gharama kubwa za huduma msingi walifunga barabara na walichoma matairi na jengo la manispaa katika kitongoji cha Thembisa kaskazini mashariki mwa mji wa kibiashara wa Johannesburg.

Maafisa wamesema watu wawili waliuawa katika ufyatuaji risasi unaodaiwa kufanywa na polisi baada ya maandamano kuanza asubuhi.

“Inadaiwa kwamba walipigwa risasi, msemaji wa polisi katika manispaa hiyo Kelebogile Thepa ameiambia AFP.

Baadaye jioni, Thepa alisema miili miwili zaidi ilipatikana karibu na mlango wa jengo lililochomwa, na kufikisha idadi ya waliofariki kufikia wanne.

Aliongeza kuwa polisi walikuwa bado hawajathibitisha sababu ya vifo hivyo na kwamba uchunguzi ulikuwa bado unaendelea.

Maandamano dhidi ya huduma mbovu hutokea mara kwa mara nchini Afrika Kusini, ambayo inakabiliana na baadhi ya viwango vya juu vya ukosefu wa ajira na uhalifu ulimwenguni.

Maandamano ya hivi karibuni yamejiri baada ya rais wa zamani Thabo Mbeki kuonya kuwa nchi hiyo inaweza kushuhudia machafuko sawa na yale yaliyotokea katika nchi za kiarabu, yaliyochochewa na ongezeko la hasira ya wananchi wasioridhika.

Mwezi uliopita, Mbeki alimshtumu mrithi wake Cyril Ramphosa kushindwa kutimiza ahadi zake za kukabiliana na umaskini uliokithiri, ukosefu wa usawa na ukosefu wa ajira, ambao umefikia kiwango cha zaidi ya asilimia 34.5, huku ukosefu wa ajira kwa vijana ukikaribia asilimia 64.

XS
SM
MD
LG