Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:12

Afrika Kusini: Polisi wawakamata watu wawili kuhusiana na shambulizi kwenye kilabu cha pombe


Polisi wa Afrika Kusini wazingira eneo la tukio ambako watu 14 waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye kilabu cha pombe mjini Soweto, Julai 10, 2022. Picha ya AFP
Polisi wa Afrika Kusini wazingira eneo la tukio ambako watu 14 waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye kilabu cha pombe mjini Soweto, Julai 10, 2022. Picha ya AFP

Polisi nchini Afrika Kusini wamesema Jumatatu kwamba wamewakamata watu wawili wanaohusishwa na moja ya mashambulizi mawili kwenye vilabu vya pombe ambayo yalisababisha vifo vya watu 19, katika mauaji ambayo yalilisisimua taifa hilo.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea kufuatia uchunguzi kuhusu shambulizi la bunduki la Jumamosi usiku kwenye kilabu cha pombe katika mji wa mashariki wa Pietermaritzburg katika jimbo la KwaZulu Natal, ambako watu wanne waliuawa na wengine wanane kujeruhiwa wakati wanaume wawili walipowafyatulia risasi kiholela wateja.

Wizara ya polisi imeeleza katika taarifa kukamatwa kwa watu hao kama hatua ya kwanza ya kuwaweka kizuizini wale wote waliopanga moja ya mauaji mabaya zaidi nchini mwishoni mwa juma.

Watu wengine 15 wakiwemo wanawake wawili, waliuawa kwa kupigwa risasi mapema Jumapili wakati wakiburudika usiku katika kitongoji cha Soweto, karibu na Johannesburg, katika tukio tofauti.

Mashambulizi ya bunduki ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini, ambayo ina moja ya viwango vya juu vya mauaji duniani, yanayochochewa na vurugu za magenge yenye silaha na ulevi wa pombe.

XS
SM
MD
LG