Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:26

Afrika Kusini kuwarejesha nyumbani wanadiplomasia wake walioko Israel


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Afrika Kusini Naledi Pandor. Picha na GCIS / AFP
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Afrika Kusini Naledi Pandor. Picha na GCIS / AFP

Serikali ya Afrika Kusini ilisema Jumatatu itawarejesha wanadiplomasia wake wote walioko Israel kutokana na wasiwasi wake kuhusu hali ya huko Gaza.

Pretoria pia imesema nafasi ya balozi wa Israel nchini humo imekuwa “zaidi na zaidi isiyoweza kutegemewa", akimtuhumu mwanadiplomasia aliyetoa "matamshi ya dharau" kuhusu watu wanaoikosoa Israel.

"Serikali ya Afrika Kusini imeamua kuwaondoa wanadiplomasia wake wote mjini Tel Aviv kwa ajili ya mashauriano," waziri katika ofisi ya rais Khumbudzo Ntshavheni, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari bila kutoa maelezo zaidi.

Watu wenye silaha kutoka kundi la Kiislamu la Palestina la Hamas walivuka mpaka wa Gaza na Israel mnamo Oktoba 7, na kuua takriban watu 1,400, wengi wao wakiwa raia, na kuwachukua mateka zaidi ya 240, kulingana na maafisa wa Israeli.

Tangu wakati huo, Israel imekuwa ikiishambulia Gaza bila kuchoka na kutuma wanajeshi wa aridini. Wizara ya afya katika eneo linaloongozwa na Hamas imesema zaidi ya watu 9,700 wameuawa, pia wengi wao wakiwa raia.

Pretoria kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono Palestina, huku chama tawala cha African National Congress (ANC) mara nyingi kikihusisha na mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Waziri wa Mambo ya Nje Naledi Pandor alisema kuwarejesha wanadiplomasia ni "ni jambo la kawaida", akiongeza wanadiplomasia hao watatoa "taarifa kamili" kwa serikali, ambayo baadaye itaamua kama inaweza kutoa msaada au kama " kweli itaweza kuendelea kuulinda uhusiano".

Awali, waziri Ntshavheni alimshutumu balozi wa Israel Eliav Belotsercovsky, kwa kutoa matamshi ya dharau kuhusu Waafrika Kusini, wakiwemo viongozi wa serikali, " wanaotoa matamshi yanayopinga mauaji ya kimbari yanayofanywa na serikali ya Israel"

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG