Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na shirika la utafiti wa Jiolojia la nchini Uingereza na shirika la hisani, Water Aid, utafiti ambao uliwasilishwa kwenye kongamano la mkesha wa siku ya maji duniani mjini Dakar, Senegal.
Shirika hilo la Uingereza la utafiti wa Jiolojia(BGS) na shirika la Water Aid, baada ya utafiti wa miaka 10 yaligunduwa kwamba Afrika ina akiba ya kutosha ya maji ya chini ya ardhi kuweza kugawa maji kwa watu wote. Hata katika maeneo yenye ukame, kulingana na mtafiti mkuu wa BGS Alan MacDonald, kunaweza kuwa na maji ya kutosha chini ya ardhi.
“Unapogundua rasimali za maji ya chini ya ardhi ni labda mara 20 ya maji tuliyo nayo katika mito ya maziwa ya Afrika. Basi ni ukweli wa kustaajabisha sana, lakini kwa sababu umefichwa mara nyingi huwa hauonekani na husahaulika”, amesema.
Hali hii pia ipo huko Turkana nchini Kenya, mojawapo ya maeneo yenye ukame zaidi barani Afrika, ambapo misafara ya ngamia huonekana kati ya vyanzo vichache vya maji.
Ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi barani Afrika, kulingana na mfumo wa tahadhari ya mapema ya njaa.
Lakini hata huko Turkana, inaonekana kuna maji chini ya miguu ya wafugaji wa ngamia. Kwa mujibu wa ripoti ya 2013, Turkana ina maji ya kutosha chini ya ardhi kuweza kuhudumia Kenya kwa kipindi cha miaka 70. Hata hivyo, utafiti wa serikali umeonyesha maji hayo yana chumvi nyingi.
Hata hivyo, kuna afueni kwa Turkana na Afrika tangu utafiti mwingine wa hivi karibuni wa shirika la BGS, kupendekeza kuwa asilimia 80 ya maji ya chini ya ardhi yanaweza kutumiwa na watu wakayanywa.
Facebook Forum