Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 17:25

Urahisi wa kupata visa moja ya kivutio cha watalii Afrika


Tembo akivuka barabara katika hifadhi ya Tarangire, Arusha, Tanzania, Jan. 16, 2015.

Afrika Kusini, Ghana na Senegal zinaripotiwa kuingiza fedha nyingi sana kutoka sekta za utalii. Ripoti iliyotolewa wiki hii inaonyesha kuwa watalii huenda wanachagua mahali pa kwenda kutokana na kwanza urahisi wa kupata visa ya kuingia nchini humo.

Ghana na Nigeria zinajulikana kama mataifa makubwa ya Afrika magharibi. Lakini moja ya tofauti zao kubwa ni katika mafanikio yao ya kuvutiwa watalii

Ripoti iliyotolewa na kundi la la London Renaissance Capital wiki hii inasema Nigeria inapata kiasi cha dolla millioni 500 katika mapato ya watalii kila mwaka, ikiwa ni asilimia 0.1 ya uchumi wa nchi hiyo ambayo ni kiasi cha dolla billioni 481.

Ghana inakusanya mapato makubwa zaidi kutoka katika sekta ya utalii. Wataalam wa London Renaissance wanasema Ghana, pamoja na Tanzania, Rwanda na Senegal ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri zaidi katika mapato ya kitalii.

Kenya ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikiongoza imeona mapato yake yakipungua katika miaka ya karibuni kutokana na vitisho vya usalama. Nigeria - pamoja na vivutio vyake vya kitalii - iko karibu na chini kabisa, juu tu ya DRC.

Nchi zote hizo zina aina fulani ya demokrasia. Lakini hilo pekee sio linalovutia watalii. Morocco na Jordan ni nchi za kifalme lakini ni miongoni mwa nchi zinazovutia sana watalii.

Nchi zenye watalii wengi pia hazina vita au vitisho vya usalama. Lakini hicho pekee sio kinachovutia watalii. Afrika Kusini ni nchi ambayo ina miji yenye viwango vikubwa vya uhalifu duniani lakini bado inavutia watalii wengi.

Tanzania na Senegal

Robertson wa London Renaissance anasema watalii wanapenda kwenda Tanzania na Senegal kwa sababu ni rahisi kuingia katika nchi hizo.

“Nyingi ya nchi zinazofanya vizuri katika utalii zina mfumo rahisi wa kupata visa,” anasema Robertson.

Rwanda hivi karibuni ilibadilisha utaratibu wake wa visa na tayari imeanza kuona faida zake, Robertson anasema.

“Wameanzisha mfumo wa visa ya wazi na wanapata asilimia nne ya pato lao taiga. Hiyo ni mara 40 zaidi ya kile inachopata Nigeria," alisema.

Robertson anasema baadhi ya nchi za Afrika zinaendelea kuwa na utaratibu mgumu wa visa kwa sababu raia wao wanapata shida sana kupata visa za kuingia katika nchi wanazotokea watalii.

XS
SM
MD
LG