Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:47

Afisa wa ngazi ya juu wa Tigray ajisalimisha


Raia wa Ethiopia wakikimbia vita Tigray wakisafiri kutumia boti kuvuka mto Setit katika mpaka wa Sudan-Ethiopia kupitia kijiji cha Hamdayet, jimbo la Kassala, Sudan.
Raia wa Ethiopia wakikimbia vita Tigray wakisafiri kutumia boti kuvuka mto Setit katika mpaka wa Sudan-Ethiopia kupitia kijiji cha Hamdayet, jimbo la Kassala, Sudan.

Afisa wa ngazi ya juu kutoka jimbo lenye mzozo la kaskazini mwa Ethiopia – Tigray amejisalimisha , vyombo vya habari vimeripoti.

Keria Ibrahim ni mmoja kati ya wajumbe 9 wa kamati kuu ya utawala wa chama cha Tigray liberation Front – TPLF ambacho wanajeshi wake wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali tangu mwezi uliopita.

Bi Keria alikuwa msemaji wa zamani wa bunge la taifa la Ethiopia kabla ya kujiuzulu mwezi juni baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Agosti kuahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Mapigano bado yanaripotiwa katika baadhi ya maeneo ya Tigray licha ya kwamba Waziri Mkuu Abiy kutangaza ushindi. Imekuwa ni vigumu kuthibitisha madai kutoka kwa serikali kuu na ile ya jimbo la Tigray kwa sababu mawasiliano yamezuiwa.

Na katika tukio jingine serikali ya Addis Ababa imefikia makubaliano na Umoja wa Matifa juu ya kupeleka msaada wa dharura katika jimbo hilo la Tigray.

Makubaliano yaliyotiwa saini na Waziri wa amani wa Ethiopia na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo yanatoa nafasi kwa umoja huo kuwahudumia watu wote wanaohitaji msaada katika jimbo la Tigray bila ya vizuizi vya aina yoyote ile.

XS
SM
MD
LG