Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 10:18

Serikali ya Ethiopia yaahidi kuwalında raia katika operesheni ya kijeshi Tigray


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewaambia wajumbe maalum wa Umoja wa Afrika serikali yake itawalinda raia, siku moja baada ya kutangaza jeshi la taifa linaanza awamu ya mwisho ya mashambulizi katika jimbo la Tigray.

Lakini taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wao, suala la mazungumzo na kundi la Ukombozi wa Watu wa Tirgay, TPLF, halikutajwa.

Serikali ilikuwa imeipatia TPLF hadi Jumatano usiku kuweka silaha zao chini au kukabiliwa na mashambulizi kwenye mji mkuu wa jimbo hilo wa Mekelle na kuzusha hofu miongoni wa wakazi nusu milioni wa mji na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Abiy kukutana na Marais wa zamani Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Joaquim Chisano wa Msumbiji na mwanasiasa wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe, imesema serikali ina dhamira ya dhati kuwalinda raia wake.

Taarifa hiyo hata hivyo haikuzungumzia juu ya mazungumzo zaidi baada ya hii leo.

Wajumbe hao walipelekwa Addis Ababa ili kusaidia katika upatanishi wa mzozo wa Tigray ambao Abiy ameeleza bayana hataki utanzuliwe na jumuia ya kimataifa.

Mgogoro huo umesababisha maelfu ya wananchi wa Ethiopia kukimbilia Sudan ambako maafisa wa huduma za dharura wanasema kambi inayowahifadi imejaa.

Na Umoja wa Mataifa inakadiria kwamba raia wa Ethiopia milioni moja laki moja watahitaji msaada wa dharura kutokana na ugomvi huo wa Tigray.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG