Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:10

Afisa mstaafu wa FBI akamatwa kwa kumfanyia kazi kwa siri tajiri wa Russia


Makao makuu ya FBI mjini Washington
Makao makuu ya FBI mjini Washington

Afisa mstaafu wa Idara ya uchunguzi ya Marekani (FBI) amekamatwa na kufunguliwa mashtaka mjini New York na Washington kwa tuhuma za kukiuka vikwazo vya Marekani kwa kumfanyia kazi kwa siri tajiri wa Russia na kupokea maelfu ya dola kutoka kwa mfanyakazi wa zamani wa idara ya ujasusi ya Albania.

Charles McGonigal, ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi cha FBI huko New York kuanzia mwaka wa 2016 hadi 2018, na Sergey Shestakov, mwanadiplomasia wa zamani wa Russia na mkalimani, walikamatwa Jumamosi mjini New York kwa ukiukwaji wa vikwazo na utakatishaji wa fedha.

McGonigal na Shestakov wanashtumiwa kwa kumchunguza tajiri mpinzani wa Russia na badala yake kupokea malipo ya siri, kulingana na shataka la tano ambalo halijatangazwa hadharani katika wilaya ya kusini mwa New York.

Katika shtaka tofauti la tisa ambalo halijatangazwa hadharani Washington DC, McGonigal anashtumiwa kupokea angalau dola 225,000 pesa taslimu kutoka kwa mfanyakazi wa zamani wa idara ya ujasusi ya Albania, wakati akisimamia juhudi za ujasusi kwa niaba ya ofisi ya FBI mjini New York.

XS
SM
MD
LG