Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, ameitaka nchi jirani ya Pakistan kumfukuza kiongozi mtoro wa Taliban kutoka kwenye ardhi yake na kumkabidhi kwa Kabul kwa ajili ya kukabiliwa na mashtaka.
Katika hotuba kali kwenye kikao cha nadra cha pamoja cha bunge la taifa leo Jumatatu, Ghani alisema viongozi wa Pakistan waliahidi watatumia nguvu dhidi ya viongozi wa Taliban ambao wanakataa kumaliza vita na kujiunga kwenye mazungumzo ya amani ya Afghanistan.
Alielezea kwamba viongozi wa waasi wanaendelea kutumia vituo vyao katika miji ya Peshawar na Quetta nchini Pakistan kwa ajili ya kuongoza ghasia Afghanistan.