Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 14:04

Afghanistan: Kundi la Islamic State lamuua mkuu wa polisi na walinzi wake wawili


Ramani ya Afghanistan

Maafisa nchini Afghanistan Jumatatu wamesema bomu lililotegwa ndani ya gari limemuua mkuu wa polisi wa jimbo na walinzi wake wawili.

Mshirika wa kundi la kigaidi la Islamic State nchini Afghanistan, IS Khorsan, lilidai kuhusika la shambulio la bomu huko Faizabad, mji mkuu wa jimbo la kaskazini mashariki wa Badakhshan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani inayoongozwa na Taliban katika mji mkuu wa Kabul, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba afisa wa polisi aliyeuawa alikuwa anaelekea kazini wakati gari hilo lililokuwa na vilipuzi lililenga gari lake.

Msemaji huyo, Abdu Nafi Takoor amesema mlipuko huo ulijeruhi pia watu wawili. Ameongeza kuwa maafisa wa polisi wamewatia mbaroni washukiwa wanne kwa kuhusiana na shambulio hilo.

Kundi la IS-Khorsan lilimezidisha mashambulizi ya kigaidi nchini Afghanistan tangu Taliban wachukue tena madaraka mwezi Agosti mwaka 2021.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG