Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:52

Senegal yaongeza matumaini katika kundi C

Wachezaji wa Afrika Kusini wakisherehekea goli lao kabla ya Senegal kusawazisha
Wachezaji wa Afrika Kusini wakisherehekea goli lao kabla ya Senegal kusawazisha

Senegal ambao walishinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Ghana sasa wanaongoza kundi C wakiwa na pointi nne, wakifuatiwa na Ghana na Algeria zenye pointi tatu kila moja. Afrika Kusini ina pointi moja.

Senegal imefanikiwa kupanda katika nafasi ya juu katika kundi gumu la C kwenye fainali za kombe la mataifa ya Africa 2015 huko Equatorial Guinea baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya 1-1 na Afrika Kusini Ijumaa.

Baada ya nusu ya kwanza ambayo haikuwa na msisimko mkubwa Afrika Kusini walitangulia kuona mlango wa Senegal sekunde chache baada ya kipindi cha pili kuanza kwa goli la Oupa Manyisa katika dakika ya 46 baada ya kupokea krossi kutoka kwa Anele Ngcongca.

Dakika 13 baadaye Kara Mbodji aliipatia Senegal bao la kusawazisha kwa kubandika kichwa kutoka krossi ya Pape Diop na kufanya ngoma sare 1-1.

Senegal ambao walishinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Ghana sasa wanaongoza kundi C wakiwa na pointi nne, wakifuatiwa na Ghana na Algeria zenye pointi tatu kila moja. Afrika Kusini ina pointi moja.

Lakini kama ilivyo katika kundi B, timu zote nne za kundi C zina nafasi ya kuweza kuingia raundi ya robo fainali kutokana na matokeo ya mechi zao za mwisho. Januari 27 Afrika Kusini inapambana na Ghana wakati Senegal inakutana na Algeria

XS
SM
MD
LG