Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:37

Sare ya DRC, Cape Verde yaweka kundi B pagumu


Afcon 20115 (DRC,Cape Verde)
Afcon 20115 (DRC,Cape Verde)

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na Cape Verde zilitoka sare katika mechi yao Alhamisi huko Ebebiyin na kufanya kundi B katika michuano hiyo kuzidi kuwa gumu.

Kwa matokeo haya huku kila timu ikiwa imebakiwa na mechi moja tu, Tunisia inaoongoza kundi ikiwa na pointi nne, ikifuatiwa na DRC na Cape Verde ambazo kila moja ina pointi mbili.

Mabingwa wa mwaka 2012 Zambia ambao walipoteza mechi yao 1-2 kwa Tunisia katika mechi nyingine ya kundi B alhamisi imebaki ikiwa na pointi moja tu iliyopata katika sare yake ya 1-1 na DRC.

Hata hivyo kila timu bado ina nafasi ya kuingia raundi ya pili endapo itashinda mechi yake ya mwisho, lakini Zambia inatumaini pia kuwa isaidiwe kwa matokeo ya timu nyingine.

Mechi za mwisho za kundi hilo zinachezwa Januari 26 ambapo DRC itapambana na Tunisia wakati Zambia itakumbana na Cape Verde. Tunisia inahitaji sare tu kuweza kuingia raundi ijayo ikiwa na pointi tano wakati DRC, Cape Verde na Zambia zinahitaji kushinda mechi zai ili kuweza kusonga mbele.

XS
SM
MD
LG