Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 19:32

ADF yadaiwa kufanya mauji ya watu 42 DRC


Shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na waasi wanaohusishwa kushirikiana na Islamic State limeuwa watu kadhaa katika mji wa Beni, mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, serikali ya mkoa huo imesema Alhamisi.

Kanali Alain Kiwewa Mitela, afisa wa mkoa huo katika eneo la Lubero ambako shambulio la usiku limefanyika ameliambia shirika la habari la AFP kwamba maiti 42 wamepatikana.

Shambulizi hilo linafikisha idadi ya watu waliouwawa na waasi wa ADF kufikia takriban 150, kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa serekali za mitaa na makundi ya kiraia.

Kiongozi wa mashirika ya kiraia, Seba Paluku, ameiiambia AFP kwamba kulikuwa na maiti 41 ikiwa ni pamoja na baadhi waliofungwa na kukatwa vichwa.

Amesema alikwenda eneo hilo na polisi na kukuta miili ikiwa imelala chini, na hakukuwa na njia ya kuisafirisha kwa sababu magari hayafiki huko, amesema.

Forum

XS
SM
MD
LG