Meya wa eneo hilo na jeshi la DRC walihusisha mauaji hayo na kundi la Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye asili ya Uganda, ambalo sasa lina makazi yake mashariki mwa Congo, ambalo limetangaza kutii kundi la wanamgambo wa Islamic State na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara.
Msemaji wa jeshi la jimbo hilo Antony Mwalushayi, alisema mashambulizi dhidi ya raia huko Oicha yanaaminika kuwa ya kulipiza kisasi mashambulizi ya hivi majuzi ya jeshi dhidi ya ADF.
Aliwaambia waandishi wa habari kwamba Washambuliaji walitekeleza mauaji hayo kwa mapanga badala ya bunduki, ili kukwepa wanajeshi waliokuwa karibu kusikia milio ya bunduki na kutambua shambulio linafanyika, .
Forum