Makubaliano hayo yaliyosainiwa tarehe 2 Novemba yaliridhia kumaliza vita vya miaka miwili ambavyo viliharibu eneo la Tigray, kuua maelfu ya watu, kuwahamisha kwenye makazi yao mamilioni ya watu na kutishia umoja wa taifa hilo la pili lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.
Serikali ya Abiy na wawakilishi kutoka Tigray Jumamosi walisaini makubaliano zaidi ya kutekeleza usitishaji mapigano.
“Tumepiga hatua moja mbele, tumejadiliana, tumekubaliana na kutia saini. Jambo la kufuata linalotarajiwa kutoka kwetu litakuwa kutekeleza kwa uaminifu kile tulichoahidi kufanya amani idumu,” Abiy ameliambia bunge la Ethiopia baada ya kusikiliza masuali ya wabunge.