Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:11

Abiria 43 wa ndege ya Singapore wasalia hospitali


Watu 43 waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Singapore, ambayo ilipata mtikisiko mkubwa na kuwajeruhi wamebaki hospitalini mjini Bangkok siku nne baada ya dharura hiyo, hospitali katika mji mkuu wa Thailand imesema Jumamosi.

Majeruhi hao wako katika hospitali tatu tofauti za Bangkok, hospitali ya Samitivej Srinakarin imesema katika taarifa.

Katika hospitali hiyo ambako majeruhi 34 wako, saba wakiwa mahututi wapo Waaustralia watatu, wawili ni raia wa Malaysia, Muingereza mmoja na raia wa New Zealand, taarifa hiyo imesema.

Wengine 27 ni pamoja na Waingereza wanane, Waaustralia sita, Wamalaysia watano, na wawili Raia wa Ufilipino, imesema taarifa hiyo.

Watu wawili waliruhusiwa kutoka hospitali wakati huku wawili wakihamishwa ili kujumuika na jamaa waliolazwa hospitali nyingine taarifa ilisema.

Abiria mmoja alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo na dazeni kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG