Gbemisola Saraki, waziri wa serikali wa uchukuzi, alisema katika taarifa Jumamosi usiku kwamba serikali ilikuwa inafanya kazi kuhakikisha abiria wote waliotekwa nyara wameachiliwa huru.
Abiria walioachiliwa huru walipelekwa katika hospitali moja mjini Abuja. Saraki hakusema jinsi gani na wapi waliachiliwa huru au ikiwa fidia ililipwa.
Magenge ya watu wenye silaha, wanaojulikana kama majambazi, walilipua njia ya reli ya Abuja-Kaduna kaskazini mwa nchi hiyo na kufyatua risasi kwenye treni ya usiku Machi 28, na kuua watu wanane.