Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 06:22

Abdel Rahim El Keeb, Waziri Mkuu mpya Libya.

.Waziri wa Ulinzi wa serikali ya mpito wa Ulinzi ya Libya Mohammed Dfeynas (kulia) akimkaribisha katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen huko Tripoli.
.Waziri wa Ulinzi wa serikali ya mpito wa Ulinzi ya Libya Mohammed Dfeynas (kulia) akimkaribisha katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen huko Tripoli.

Baraza la mpito la taifa lachagua waziri mkuu mpya ambaye ana kazi ya kuunda serikali mpya.

Baraza la mpito la taifa la libya NTC limemchagua Abdel Rahim el keeb kama waziri mkuu mpya saa chache kabla ya NATO kumaliza operesheni zake huko Libya.

Mkazi huyo wa Tripoli alipata ushindi mdogo, akipata kura 26 kati 51 za wanachama wa baraza la mpito la taifa.

El Keeb alisomea hapa Marekani uhandisi wa umeme ambaye alipata shahada ya udaktari katika chuo kikuu cha North Carolina.

Amepewa jukumu la kuunda serikali mpya ambayo itafungua njia kwa uchaguzi mkuu.

XS
SM
MD
LG