Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:12

Abbas atishia kujitoa katika mazungumzo


Kiongozi wa Palestina amwonya Obama atajitoa katika mazungumzo ya amani kama Israel haitatekeleza masharti yake.

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas amemtahadharisha rais Barack Obama wa Marekani kuwa Wapalestina watajitoa katika mazungumzo ya amani na Israel endapo taifa hilo la Kiyahudi litasitisha upunguzaji wa ujenzi wa makazi ya watu katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ng'ambo ya Magharibi.

Mjumbe Mkuu wa Palestina Saeb Erekat aliwaambia waandishi mjini Ramallah Jumatatu kuwa Bwana Abbas amemtumia barua rais Obama akisisitiza kuwa ujenzi ukianza kwa kasi tena mazungumzo hayo yatavunjika.

Mazungumzo ya amani ya Israel na Palestina yanatazamiwa kuanza tena mjini Washington Septemba 2. Ujenzi wa makazi ya watu Ng'ambo ya Magharibi imekuwa moja ya maswala yenye mvutano mkubwa.

Israel ilipunguza kasi ya ujenzi huo kwa miezi 10. Lakini muda wa kupunguza kasi hiyo unatazamiwa kwisha mwishoni mwa Septemba na serikali ya Israel imegawanyika endapo endelee kupunguza ujenzi au urejee katika kiwango cha kawaida.

XS
SM
MD
LG