Tume ya uchaguzi ya Ivory Coast imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya orodha ya wapiga kura kwa uchaguzi wa mwaka ujao wa urais ambao mara kwa mara umecheleweshwa.
Maafisa wa uchaguzi walitangaza Jumanne kuwa wamesogeza mbele tarehe ya mwisho kuchunguza upya orodha ya wapiga kura kwa siku 10 hadi Januari sita.
Tume hiyo inasema imeshughulikia kiasi cha asilimia 40 ya malalamiko na wanahitaji muda zaidi kukamilisha kazi yao.
Maafisa wanasema hatua hiyo haiwezi kuchelewesha uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Februari mwishoni au mapema Machi ya 2010.
Ivory Coast imekuwa ikichelewesha uchaguzi wa rais mara kadhaa tangu mwaka 2005, hasa kwa sababu ya mizozo juu ya nani anastahili kupiga kura.
Rais Laurent Gbagbo ameomba uvumilivu, akisema ni bora kuchelewesha kura kuliko kuwa na mifarakano au vifo.