Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:50

Habari kuu za wiki Kenya na Marekani


Vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa viliangaza sana ziara ya mpatanishi mkuu wa mgogoro wa kisiasa wa Kenya bwana Kofi Annan ambaye zamani alikuwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa. Bwana Annan alikutana na Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga kushinikiza serikali itekeleze mabadiliko yaliyofikiwa ya mkataba wa kitaifa ambapo serikali ya mseto iliundwa. Akizungumza na sauti ya Amerika, mwandishi habari wa gazeti la Daily Nation huko Kenya Douglas Mutua, alisema ingawa bwana Annan alikaribishwa rasmi na serikali kulionekana kuibuka utengano mkubwa hata kabla ya Annan kuondoka nchini humo. Bwana Annan aliashiria kuwa angependa kuzuru Kenya tena mwezi Disemba. Bwana Mutua aliilinganisha serikali hiyo ya mseto na vigae vya chungu kikubwa kilichovunjika akieleza kuwa wanasiasa wa chama cha ODM cha bwana Odinga kilisema kitamkaribisha kama mgeni wao huku kile cha bwana Kibaki PNU kikisema kuwa bwana Annan anaweza kurejea Kenya kama mtalii. Naye mwandishi habari na mchambuzi wa maswala ya kisiasa hapa Marekani, bwana Mobhare Matinyi alieleza changamoto zinazokabili utawala wa rais Barack Obama nchini Afghanistan ambapo wanamgambo wa Taliban wanadhibiti asili mia 80 ya nchi wakitumia falsafa kwamba wanajaribu kukomboa nchi yao kutokana na ukaliaji wa majeshi ya Marekani. Bwana Matinyi anasema wanajeshi hao ambao wamejiondoa kwenye maeneo ya milimani wanakabiliana na changamoto kubwa ya wapiganaji wa Taliban ambao hufanyia mafunzo yao nchini Pakistan katika mkoa wa Waziristan na kuvalia kama raia bila kujipanga wala kutumia silaha za kisasa. Na kuhusu kura ya jumanne ya mswada wa mabadiliko ya afya hapa Marekani bwana Matinyi anasema kuna uwezekano mkubwa kwa rais Obama kupata ushindi na kufanya mabadiliko ambayo amekuwa akiyanadi kwa muda wa miezi kadhaa sasa.

XS
SM
MD
LG