Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:57

Kenya yakumbwa na Njaa


Kutokana na hali mbaya ya ukame watu wasiopungua milioni 10 nchini Kenya wanakabaliwa na uhaba wa chakula. Mwandishi wa sauti ya Amerika huko Nairobi, anaripoti kuwa hali hiyo imepelekea matatizo mengine kama vile ukosefu wa nguvu za umeme.

Serikali kupitia kampuni ya umeme imetangaza mgao wa umeme wa nchi nzima jambo ambalo litasababisha madhara makubwa kwa karibu sekta zote za uchumi.

Baadhi ya viwanda vimeanza kufungwa na vijana wengi kupoteza ajira, bei ya mafuta ya petroli imepanda ikiwa ni pamoja na nauli za usafiri. Pia kutokana na kuzorota kwa hali ya uchumi duniani baadhi ya mabenki na taasisi za fedha zimeanza kuongeza riba wanayotoza kwa mikopo.

Wakati huko mashambani mimea inakauka na wakulima hawana matumaini yeyote ya kuvuna huku baadhi yao wakisema hawajaona njaa kama hii. Wakazi wa mijini wanajiuliza ni kipi cha kununua kati ya maji na Unga. Rais Kibaki ametangaza msiba wa kitaifa huku wafanya biashara wamepewa ruhusa ya kuagiza chakula kutoka nje.

XS
SM
MD
LG