Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 18:36

Ajali ya treni Dodoma


Nchini Tanzania kulitokea ajali ya treni siku ya Jumapili kwenye eneo la Msagali wilayani Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma. Ajali hiyo ilihusisha treni ya mizigo na abiria kutoka Dar-es-salaam kuelekea Bara, ambapo watu saba walifariki na wengine kujeruhiwa. Taarifa zinasema dereva wa treni ya mizigo alisimama katika eneo hilo bila kutoa taarifa yeyote kwa madereva au wafanyakazi wenzie na mara treni ya abiria ilipowasili eneo hilo mabehewa yaligongana na kusababisha vifo katika ajali hiyo. Hata hivyo baadhi ya wananchi katika eneo hilo wanasema ajali hiyo ni njama za makusudi zinazofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Reli ili kuiba mafuta kutoka kwenye mabehewa ya mizigo. Tayari madereva na wafanyakazi wengine kadhaa wa shirika la reli wanashikiliwa na polisi kusaidia uchunguzi wa ajali hiyo. Mkamiti Kibayasi alizungumza na mkuu wa mkoa wa Dodoma bwana William Lukuvi.

XS
SM
MD
LG