Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 03:25

Kura ya maoni Comoros


Huko nchini Comoro wananchi wamepiga kura ya maoni Jumapili juu ya mabadiliko ya katiba ya visiwa hivyo ambayo yatampa rais wa nchi hiyo muda wa ziada kushikilia madaraka badala ya kisiwa cha Mwale. Mwenyekiti wa chama cha Kasi ya Comoro Mohamed Mshangama ambaye pia aliwahi kuwa spika wa bunge ameelezea wasi wasi wake na kudai kwamba rais wa nchi hiyo Bw.Sambi anataka kuchukua madaraka yote peke yake na amedai pia kuwa kura hiyo iliandikwa kwa kifaransa kigumu sana ambacho mwananchi wa kawaida hawezi kuelewa. Aidha aliongeza kuwa makubaliano ya uongozi wa rais yalikuwa ya kubadilishana kila kisiwa lakini Bw.Sambi hataki kutekeleza makubaliano hayo na anataka kuendelea kushikilia madaraka. Akizungumzia kuhusu upigaji kura huo amesema watu waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni walikuwa ni chini ya asilimia 10 ya wananchi wa visiwa hivyo akidai kuwa raia wa nchi hiyo wana wasiwasi mkubwa kwasababu ya uwepo wa majeshi kote visiwani humo.

XS
SM
MD
LG