Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 04:22

Vipimo vya HIV Kenya


Serikali ya Kenya imesema inasubiri utafiti wa miradi mingine ili kubaini kama maelfu ya watu kutoka Kenya na uganda waliofanyiwa vipimo vya HIV walipewa matokeo yasiyo sahihi.Utafiti unaonyesha kuwa watu zaidi ya elfu sita waliopimwa virusi vya HIV katika vituo vya VCT wengi waligunduliwa wamepata virusi vya HIV wakati hawana na kukiwa na uwezekano kwamba vipimo vingine vinaonyesha kutoathiriwa wakati kuna maathiriko.Mkuu wa mipango maalum katika idara ya Ukimwi kutoka ofisi ya rais Joshua Ng'e lo alizungumza nasauti ya Amerika kuhusu jambo hilo. Vipimo hivi vilifanywa kati wa watu wenye umri wa miaka 18-60 na Bw,Ng'e lo alipoulizwa kwenye mahoijiano haya alisema haijawahi kutokea siku za nyuma na kwamba binadamu ni binadamu inaweza kuwa makosa ya kibinadamu na Kenya ina vituo zaidi ya elfu moja vya VCT ambavyo vinapima watu zaidi ya laki nane kwa mwaka.Alielezea zaidi kuwa serikali inahakikisha kabla ya kujengwa vituo vibali havitolewi mpaka wahakikishe kuwa wafanyakazi wa vituo hivyo wamehitimu na wana ujuzi wa kutosha kutimiza wajibu wao.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG