Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 02:04

Chuo cha Kenyatta Chafungwa


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, jumatano waligoma na kufukuzwa chuoni.Wanafunzi hao baadaye waliingia katika barabara kuu ya Nairobi kuelekea Thika na kuvurumishia magari mawe na kufanya uharibifu mkubwa kabla ya kutawanywa na maafisa wa polisi.Akizungumza na sauti ya Amerika, mhadhiri katika chuo hicho, Profesa Geoffrey Kitula King’ei alisema kero la wanafunzi hao lilikuwa kuamrishwa waondoke chuoni, baada ya kushindwa kulipa karo na kujiandikisha ipasavyo kwa muda uliotolewa na chuo hicho.Profesa Kinge’i alisema wanafunzi hao walitaka muda wa kulipa karo na kujiandikisha uongezwe licha ya kuwa tarehe ya mwisho ilikuwa februari 13. Aidha Profesa King’ei alisema chuo kikuu cha Kenyatta kimesimama kidete kuwa sharti wanafunzi hao waondeke na kurejea chuoni watakapotimiza maagizo ya chuo hicho.
XS
SM
MD
LG