Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:37

Obama aahidi hatua zaidi dhidi ya Ugaidi


Rais wa Marekani Barack Obama amesema Marekani itatumia kila kipengele ndani ya uwezo wake ili kuzuia, kuharibu na kushinda ugaidi popote duniani ambao utataka kushambulia Marekani.

Bw. Obama alikua akiznugumzakutoka Hawaii Jumatatu, na muda mfupi baadaye tawi la Al Qaida huko Yemen lilisema linahusika na jaribio la Ijumaa la ndege ya North West kutoka Amsterdam kwenda Detroit.


Taarifa ya mtandao inayodhaniwa kuwa ya Al Qaida katika rasi ya Arabia imesema, shambulizi hilo lilikua ni majibu kwa juhudi za Marekani dhidi ya kundi hilo la wanamgambo huko Yemen. Vyombo vya habari vya Marekani vimewakariri viongozi wa serikali wakisema Marekani imekuwa ikiipa Yemen wakufunzi wa kijeshi na silaha kupambana na Al Qaida.

Bw.Obama amesema Marekani inafanya kila kitu kuwalinda raia wake na imeimarisha usalama. Amesema serikali pia inaangalia upya hatua za usalama ikiwa ni pamoja na orodha ya kuwaangalia magaidi katika juhudi za kuzuia mashambulizi yajayo.


Umar Farouk Abdulmutallab, raia wa ki-Nigeria mwenye umri wa miaka 23, ameshitakiwa kwa kujaribu kulipua ndege ya Northwest kwa kujaribu kutegua malipuko wakati ndege hiyo ilipokuwa ikikaribia kutua. Lakini bomu hilo lilishindwa kulipuka.

XS
SM
MD
LG