Ikiwa uchaguzi umekaribia huko Tanzania tume ya uchaguzi Zanzibar imesitisha zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa madai ya vurugu zinazofanywa na wananchi wanaotaka kuandikishwa ambao wengi wao ni wanachama wa chama cha wananchi CUF. Akizungumza na Sauti ya Amerika mbunge wa Konde kwa tiketi ya CUF Bw. Ali Taarab alisema kwamba vijana wengi wamejitokeza kudai haki yao. Na kwa takwimu zao anasema wapiga kura wamepunguzwa aidha amesema wamepeleka barua ya malalamiko yao kwa waziri kiongozi,spika wa bunge,waziri mkuu na hakuna lolote lililofanyika. Nao wananchi kadhaa wa Konde pia walielezea malalmiko yao kuwa wameshindwa kuandikishwa bali wameambiwa lazima wawe na vitambulisho vya ukazi wa Zanzibar ambavyo upatikanaji wake umekuwa na urasimu wa hali ya juu.