Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 18, 2025 Local time: 01:42

Rajoelina:Kuna fursa ndogo ya mafanikio na upinzani


Rajoelina:Kuna fursa ndogo ya mafanikio na upinzani
Rajoelina:Kuna fursa ndogo ya mafanikio na upinzani
<!-- IMAGE -->

Kiongozi wa muda wa Madagascar Andry Rajoelina anasema anaamini kuna fursa ndogo ya mafanikio kwa mazungumzo yake na Rais aliyeondolewa madarakani katika kuunda serikali ya umoja. Akiongea na waandishi wa habari huko Afrika kusini, Alhamisi wakati wa mapumziko katikati ya mashauriano, Andry Rajoelina mwenye umri wa miaka 35 amesema Rais wa zamani Marc Ravalomanana anataka mambo mengi ambayo hawezi kuyakubali.

Viongozi kusini mwa Afrika wanajaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa wa Madagascar ulioibuka mwaka jana wakati bwana Rajoelina alipochukua madaraka kwa njia ya mapinduzi akiungwa mkono na jeshi.

Katika taarifa ya Alhamisi bwana Ravalomanana alieleza kwamba mazungumzo yataendelea. Alisema anaingia katika siku ya pili ya mazungumzo yasiyo na masharti isipokuwa yale yaliyohitajika kuzungumziwa kuhusu uchaguzi huru na haki nchini Madagascar.

Mwezi Agasti mwaka jana bwana Rajoelina alikubali mkataba wa kushirikiana madaraka na viongozi kutoka makundi matatu ya upinzani nchini humo ikiwemo kundi moja lililoongozwa na bwana Ravalomanana. Hata hivyo mkataba huo baadae haukuweza kuafikiwa. Bwana Rajoelina alikataa mkataba huo mwezi Disemba.Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anaongoza mazungumzo hayo wiki hii katika mji mkuu wa Afrika kusini, Pretoria.

XS
SM
MD
LG