Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 13:04

Marekani kuisaidia Kenya shilingi milioni 157 za katiba mpya


Marekani kuisaidia Kenya shilingi milioni 157 za katiba mpya

Serikali ya Marekani imesema itaisaidia serikali ya Kenya msaada wa shilingi milioni 157 kugharamia matumizi ya kura ya maamuzi kuhusu katiba mpya nchini humo. Fedha hizo zitatumika kuwaelimisha wananchi umuhimu na kutoa mafunzo kwa wapiga kura.

<!-- IMAGE -->

Ikiwa imesalia miezi michache kabla ya nchi hiyo kuingia kwenye kura ya maamuzi kuhusu rasimu ya katiba mpya kampeni kali imeshika kasi kote nchini humo kuwasajili wapiga kura ili washiriki kwa wingi kwenye kura ya maamuzi.
Serikali ya Kenya kwa upande wake imesitisha mazungumzo ya faragha na madhehebu ya dini kuhusu vifungu vyenye utata kwenye rasimu ya katiba. Huu ni wakati ambapo wapiga kura nchini Kenya wataamua iwapo wataunga mkono au wanapinga katiba mpya nchini humo.

Balozi wa Marekani nchini Kenya bwana Michael Raddenburg, anasema ni muhimu kuzingatia ukweli sahihi uliomo kwenye rasimu ya katiba mpya badala ya kueneza uwongo na porojo zisizo za kweli wakati wa kujadili rasimu hii ya katiba mpya.

XS
SM
MD
LG