Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:35

Chama tawala Ethiopia chashutumu kiongozi wa upinzani


Chama tawala Ethiopia chashutumu kiongozi wa upinzani
Chama tawala Ethiopia chashutumu kiongozi wa upinzani

Chama tawala cha ethiopia kimesema kiongozi mmoja wa upinzani ametoa wito wa kuipindua serikali kwa nguvu, tuhuma ambazo kiongozi wa upinzani amezikanusha.

Katika taarifa iliyotolewa jumatatu chama tawala cha EPRDF kimesema Beyene Petros alitoa hotuba ambayo ilisema umma unaweza kutumia ghasia kuipindua serikali ambayo imeshindwa kutekeleza ahadi zake.

Chama hicho kilisema hotuba hiyo ilipinga katiba ya Ethiopia na ilikuwa na lengo la kuandaa ghasia.

Beyene alikanusha tuhuma hizo katika mahojiano ya leo na shirika la habari la utangazaji la kimataifa- Reuters.

Shirika hilo lilimnukuu akisema kuwa alikuwa akizungumzia taratibu za demokrasia za kawaida, na kwamba hakuwa na nia ya ghasia katika hotuba yake.

Beyene ni mwenyekiti wa muungano wa vyama vya siasa vya upinzani.

XS
SM
MD
LG