Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:17

Marekani kuimarisha ushirikiano na mataifa ya Kislamu


Marekani kuimarisha ushirikiano na mataifa ya Kislamu
Marekani kuimarisha ushirikiano na mataifa ya Kislamu

<!-- IMAGE -->

Akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa siku mbili wa viongozi wajasiriamali kutoka mataifa yenye waislamu wengi siku ya Jumanne, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton ametangaza miradi kadhaa yenye lengo la kuwasaidia wajasiriamali kutoka mataifa yenye waislamu wengi na hatimaye amesema miradi hiyo itapanuliwa ili kunufaisha mataifa mengine.

“Nina furaha ya kutangaza kuzinduliwa kwa mpango wa kwanza wa majaribio ya wajasiriamali duniani huko Misri, utakao ratibiwa na kundi la wajasiriamali waliosaidiwa na USAID. Karibuni tutazindua mradi wa pili huko Indonesia na tuna mpango wa kupanua hadi kwa mataifa12 mnamo miaka miwili ijayo.”

Mipango hiyo mipya inanuia kupanua uwezo wa kupata fedha ili wafanyabiashara wadogo waweze kupata mikopo kuwawezesha kutekeleza kazi na ndoto zao.

Bi Clinton pia alitangaza ushirika mpya baina ya shule za biashara za hapa Marekani na taasisi za elimu kote duniani ili kueneza na kupanua elimu ya biashara.

<!-- IMAGE -->

Mpango mwingine utakua wa kuwaaunganisha wataalamu wa kimarekani na wale wanaotaka kujihusisha katika biashara ndogo ndogo ili waweze kuwapata utaalamu kuhusu masuala kama vile namna ya kupata fedha au kuandika mipango ya biashara.

“Juhudi hizi ni wimbi la kwanza la miradi ya kuhamasisha ujasiriaimali duniani, lakini zinamulika nia ya utawala wa Obama kuchukua mwelekeo mpya wa maendeleo, itakayokuwa chini ya misingi ya uwekezaji na wala si msaada, kusaidia uongozi wa vijiji na miji kutekeleza mawazo badala ya kulazimisha mawazo yetu wenyewe.”

Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 250 kutoka mataifa 50 yenye waislamu wengi. Mkutano ujao wa viongozi wajasiriamali utafanyika Uturuki hapo mwakani.

XS
SM
MD
LG