Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:14

Rais wa Sudan ziarani Misri


Rais wa Sudan ziarani Misri

<!-- IMAGE -->

Rais wa Sudan Omar Al-Bashir amesafiri kwenda Misri ikiwa ni jaribio lake la karibuni kuonyesha kukaidi waranti ya mahakama ya kimataifa ya kutaka akamatwe.

Bw. Bashir alikutana na Rais wa Misri Hosni Mubarak siku moja baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi huu wa kiti cha urais nchini Sudan.

Misri imemkaraibisha Rais huyo wa Sudan mara kadhaa katika siku za nyuma licha ya mashitaka yanayomkabili katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC kwa tuhuma za uhalifu wa vita katika mkoa wa Darfur nchini sudan.

Jumatatu Bw.Bashir aliahidi kuheshimu makubaliano ya amani ya 2005 ambayo yalimaliza vita vya Sudan kusini na kaskazini na kusema kura ya maoni kwa uhuru wa kusini itafanyika kama ilivyopangwa.

XS
SM
MD
LG