Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 03:49

ICC imekataa juhudi mpya za kumshtaki Bahar


ICC imekataa juhudi mpya za kumshtaki Bahar

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC imekataa juhudi mpya za waendesha mashtaka kumshtaki kiongozi wa uasi wa Darfur kwa uhalifu wa vita.

Waendesha mashtaka wa mahakama walipinga uamuzi wa majaji kutomshtaki Bahar Idriss Abu Garda, ambaye wanasema alisaidia kupanga mauaji ya walinda amani wa Umoja wa Afrika 12 mwaka 2007.

Mahakama ilieleza Jumatatu kwamba madai ya waendesha mashtaka hayakidhi ombi la kukata rufaa. Katika uamuzi wake wa awali mwezi Februari mahakama ilisema kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuamini Abu Garda anaweza kuhusika na mauaji ya vifo vya walinda amani.

XS
SM
MD
LG