Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:50

Matumizi ya maji ya mto Nile yazusha ugomvi mpya


Matumizi ya maji ya mto Nile yazusha ugomvi mpya
Matumizi ya maji ya mto Nile yazusha ugomvi mpya

Mkutano wa waatalamu wa mkataba wa Nile Basin Initiative, wameshindwa kukubaliana juu ya matumizi ya maji ya mto Nile. Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Shimelis Kemal, anasema Misri inatoa sababu za kiufundi ili kuzuia kutiwa saini makubaliao mapya ya matumizi ya maji ya mto Nile.

Anasema nchi 7 kati ya wanachama 9 wa mkataba wa Nile Basin watatia saini mkataba huo mwezi ujao hata kama Misri na Sudan hazitashiriki.

"Washirika wa mkataba huu wanahisi Misri inatumia mikakati ya kuchelewesha ambayo imerudisha nyuma utaratibu wa majadiliano".

Mkataba wa Nile Basin Initiative ulianzishwa mwaka 1999 ili kuweza kutayarisha na kukubaliana juu ya mpango wa kisheria wa kugawanya kwa usawa matumizi ya maji ya mto Nile .

<!-- IMAGE -->

Nchi ambazo mto unamalizikia upande wa kaskazini kwa muda mrefu zimekua zikibisha kwamba mikataba mwili ya enzi za ukoloni imezipatia kwa njia isiyo ya usawa Misri na Sudan haki maalum za kipekee kutumia takribani maji yote ya mto huo mrefu kabisa duniani.

Lakini maendeleo ya mkataba mpya yamekua yakiendelea pole pole na mkutano wa wiki iliyopita katika mji wa mapumziko wa Sharm el-Sheikh nchini Misri uliolenga kumaliza vipengele vya mwisho unaripotiwa umemalizika bila ya kufikia makubaliano.

Hii imepelekea nchi 7 zilizo upande wa mto Nile unakoanza, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Rwanda, Burundi, Kenya, Tanzania na Ethiopia, kutangaza zitaendelea na sherehe za kutia saini hapo Mei 14 mjini Kampala.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia Shimelis anasema mkataba umeacha wazi kipengele chenye utata juu ya usalama wa maji kwa matumaini Misri na Sudan zitaweza kushawishika kurudi kwenye meza ya mazungumzo.

"Pande zote zimekubaliana kutilia maanani maslahi ya Misri. Makubaliano yeyote yatakayoitenga Misri hayatakua na maana hivyo wamekubaliana kujaribu kukubali maslahi ya Misri pia."

Kwa upande mwingine msemaji wa serikali ya Misri alikaririwa wiki hii akionya kwamba mkataba wowote utakaotiwa saini bila ya kuwepo Misri na Sudan utamaanisha kuvunjika kwa mkataba wa Nile Basin Initiative.

Shirika la habari la Ufaransa lilimkariri waziri wa maji wa Misri akisema sehemu ya Misri ya maji ya mto Nile ni haki ya kihistoria ambayo imetetewa wakati wote wa historia yake.

XS
SM
MD
LG