Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 30, 2020 Local time: 07:56

Jeshi la Rwanda limewakamata majenerali waandamizi

Jeshi la Rwanda limewakamata majenerali waandamizi

<!-- IMAGE -->

Jeshi la Rwanda limesema limewakamata majenerali wawili wa vyeo vya juu kwa tuhuma za rushwa na utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na naibu mkuu wa zamani wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur nchini Sudan.

Jeshi limesema limemkamata naibu mkuu wa zamani Meja Jenerali Emanuel Karenzi Karake kwa tabia ambayo inakiuka misingi ya jeshi la Rwanda.

Msemaji wa Jeshi Jill Rutaremara amesema maafisa pia wamewakamata mkuu mpya wa jeshi la akiba la Rwanda Luteni Jenerali Charles Muhire.

Muhire anatuhumiwa kwa rushwa na kutumia vibaya madaraka.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG