Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:47

Nusu ya safari za ndege kuanza tena: EU


Nusu ya safari za ndege kuanza tena: EU
Nusu ya safari za ndege kuanza tena: EU

Makao makuu ya Umoja wa Ulaya yamesema safari za ndege huko Ulaya huwenda zikarudi kufikia asilimia 50 ya kiwango cha kawaida hapo Jumatatu ikiwa utabiri wa hali ya hewa utathibitisha kwamba anga ya bara hilo haina tena jivu la volcano.

Mawaziri wa uchukuzi wa mataifa ya Ulaya yaliyoathirika na jivu la volcano kutoka huko Iceland watakutana Jumatatu kupitia mawasiliano ya video katika juhudi za kufungua tena usafiri wa ndege.

<!-- IMAGE -->

Jivu hilo la volcano limesababisha mtaharuku mkubwa wa usafiri katika kanda hiyo na maeneo mengine ya duniani kwa kufutiliwa mbali safari zote za ndege kuelekea bara la Ulaya kwa siku ya nne mfululizo. Hali hiyo imesababisha maelfu ya abiria kukwama katika viwanja mbali mbali vya ndege duniani pamoja na kuvuruga bisahara.

Kamishna wa usafiri wa Ulaya Siim Kallas, amesema Ulaya haijapata kushuhudia mzozo mkubwa wa kusitisha safari za ndege kama huu unaoendelea hivi sasa na kwamba maafisa wanalazimika kuchukua hatua za haraka kurudisha hali kua ya kawaida.

Jivu la volcano huwa na mawe, vichembechembe vya chupa, na vifaa vingine ambavyo vinaweza kusababisha injini ya ndege kukwama. Baadhi ya maafisa wa safari za ndege wamekosoa hatua za kuzuia safari zote za ndege wakitoa hoja kwamba uwamuzi ulichukuliwa kwa kutegemea mifano ya komputa pekee.

Mashirika ya ndege, KLM ya Uholanzi, Air France ya Ufaransa na Lufthansa ya Ujerumani yamefanya majaribio ya safari za ndege bila abiria mwishoni mwa wiki na marubani wao wanasema hawakukabiliwa na matatizo yeyote.

Wachambuzi wanasema mashirika ya ndege yanapoteza kiasi cha dola milioni 200 kwa siku kutokana na kusitishwa safari za ndege huko Ulaya.

XS
SM
MD
LG