Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 20:58

Mataifa ya Afrika yahimizwa kuchukua hatua kukabiliana na majanga


Mataifa ya Afrika yahimizwa kuchukua hatua kukabiliana na majanga
<!-- IMAGE -->

Mawaziri wanaoshughulika na majanga na mazingira barani Afrika wamehimizwa kutenga sehemu fulani ya bajeti ya matumizi ya nchi kwa ajili ya kupunguza maafa wakati majanga yanapotokea.

Mkutano huo unaodhaminiwa na Umoja wa Mataifa na kusimamiwa na Umoja wa Afrika unahudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa 42 ya Afrika pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyo ya kiserikali. Wajumbe wanajadili na wataidhinisha mpango wa utekelezaji kwa ajili ya mkakati wa Afrika wa kupunguza hatari za majanga na hatua kabambe kwa kipindi cha 2006 hadi 2015.

Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu Rais anayehusika na mazingira nchini Tanzania, Dr.Batilda Buriani, amesema wataalamu wametoa ripoti ya baraza la kimataifa la wanasayansi inayoonesha kabisa kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa kumetokea matukio mengi sana ya maafa. Wataalamu wamesema kuanzia miaka ya 1900 mpaka miaka ya 1940 matukio yalikuwa kama 630. Lakini kufikia mwaka 1998 matukio yalifika elfu mbili.

Dr. Buriani amesema washiriki wote wanakiri kwamba mvua zinapozidi kuongezeka na mafuriko yanapotokea ama kunapokuwa na ukame ukasababisha njaa na watu kufa ni matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema japokuwa majanga mengine ni ya asili lakini pia yapo yale yanayosababishwa na binadamu kama uharibifu wa mazingira unaotokana na kuchoma misitu ovyo. Amesema suala la majanga linaumiza kila sekta na ni changamoto kubwa kwa nchi yake na kuna vielelezo tosha vya kueleza jinsi gani Tanzania ilivyoathirika mfano theluji ya mlima Kilimanjaro asilimia 80 imeshapotea na maeneo mengi ya ufukwe yameathiriwa.

XS
SM
MD
LG