Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:54

Uchaguzi wamalizika Sudan


Uchaguzi wamalizika Sudan
Uchaguzi wamalizika Sudan

<!-- IMAGE -->

Upigaji kura nchini Sudan umemalizika Alhamisi baada ya siku tano za uchaguzi ambao uligubikwa na matatizo ya uendeshaji na tuhuma za udanganyifu.

Vituo vya kupigia kura vinafungwa saa kumi na mbili jioni na kura zinatarajiwa kuanza kuhesabiwa Ijumaa.

Uchaguzi huo wa kwanza wa vyama vingi tangu 1989 ulikua ni wa Rais, wabunge na madiwani. Wafuatiliaji wa uchaguzi wa kimataifa hawajatoa taarifa rasmi kuhusu uchaguzi huo.

Hata hivyo walioshuhudia wanasema upigaji kura ambao ulikuwa wa amani ulikumbwa na matatizo kadhaa ikiwa ni pamoja na utata wa karatasi za kupigia kura na majina kukosekana kwenye karatasi za kupigia kura, vituo kuchelewa kufunguliwa na katika baadhi ya maeneo kulikuwa na ukosefu wa vifaa.

Vyama kadhaa vvya upinzani vimejitoa moja kwa moja ama kushiriki kwa kiwango kidogo vikisema kuwa Rais Omar al-Bashir na chama chake kinachotawala cha National Congress walipanga kuvuruga matokeo.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema udanganyifu hautakuwepo katika uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG