Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 10:17

Muda wa uchaguzi Sudan unaongezwa


Muda wa uchaguzi Sudan unaongezwa
<!-- IMAGE -->

Tume ya taifa ya uchaguzi ya Sudan imeongeza muda wa kupigaji kura kwa siku mbili katika upigaji kura wa kitaifa wa kwanza kwa karibu robo karne.

Upigaji kura huo ambao ulianza Jumapili umegubikwa na matatizo ya kiufundi na ucheleweshaji katika vituo vya kupigia kura hasa kwa Sudan Kusini.

Upigaji kura wa kiti cha urais na bunge ambao mwanzo ulipangwa kumalizika Jumanne sasa utaendelea hadi alhamis wiki hii.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani P.J Crowley amesema serikali ya Khartoum inaweza kufanya zaidi kuunda kile alichokiita “hali muafaka ya uchaguzi”.

Lakini amesema Marekani inaangalia kura hiyo kama hatua muhimu katika mpango wa amani wa nchi hiyo.

Na Khadija Riyami amezungumza na Mwamoyo Hamza aliyeko huko Sudan Kusini na anaeleza kuwa watu wamefurahi baada yua siku za kupiga kura kuongezwa na kwamba shida kubwa ni uzoefu wa namna gani wapige kura na uendeshaji mzima wa zoezi hilo.

Na akielezea kuhusu ushiriki wa wanawake amesema maeneo ya mijini ni wengi waliojitokeza lakini kwa maeneo ya vijijini bado ni vigumu kuelewa hali halisi ikoje.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG