<!-- IMAGE -->
Wananchi wa Sudan walipiga kura Jumapili katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi katika miaka 24.
Kulikuwa na ripoti za kupotea kwa kura kuchelewa kwa kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura na kukanganyikiwa kati ya wafanya kazi wa vituo vya kupigia kura na wapiga kura katika siku tatu za kupiga kura.
Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika akiripoti kutoka Juba Sudan Kusini anasema baadhi ya wafanyakazi wa vituo vya kupigia kura walihamishwa kwenye vituo vipya bila taarifa.
Mashahidi wanasema baadhi ya wapiga kura walikanganyikiwa na kura tofauti kwa rais wabunge na ofisi za majimbo na kanda. Awali waliojitokeza kupiga kuwa walikuwa wachache.