Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:35

Raia wa Poland waomboleza vifo vya viongozi wao


Raia wa Poland waomboleza vifo vya viongozi wao
Raia wa Poland waomboleza vifo vya viongozi wao
<!-- IMAGE -->

Maelfu na maelfu ya raia wa Poland wamekua wakitoa heshima zao za mwisho nje ya ikulu ya rais mjini Warsaw, wakiombolezavifo vya rais Lech Kaczynski, mkewe Maria, na watu wengine 95, wakiwemo maafisa wa vyeo vya juu wa serikali.

Mwili wa rais ulirudishwa Warsaw Jumapili, na umewekwa ikulu kwa watu kutoa heshima zao za mwisho.

Rais Kaczynski, alifariki katika ajali ya ndege magharibi ya Rashia siku ya Jumamosi. Kiongozi huyo aliyekua na umri wa miaka 60 aliuwawa wakati ndege yake ya aina ya Tupolev TU 154 ilipoanguka ikikaribia uwanja wa ndege karibu na Smolensk.

Miongoni mwa abiria walouwawa ni pamoja na mke wa rais, Maria, mkuu wa majeshi wa Poland, naibu waziri wa mambo ya kigeni, gavana wa benki kuu, na wabunge kadha wa Poland. Gavana wa jimbo la Smolensk anasema hakuna aliyenusurika kati ya watu 97 walokua ndani ya ndege hiyo.

Ujumbe huo wa serikali ya Poland ulikua unaelekea katika mji wa magharibi wa Rashia Smolensk, kuudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 70 tangu mauwaji ya maafisa 22,000 wa Poland walouliwa na vikosi vya usalama vya Urusi wakati wa vita vikuu vya kwanza.

Bw Kaczynski alichaguliwa rais wa Poland 2005. Mwaka mmoja baadae, alitangaza mipango yake ya kuifanya Poland kua mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Akisema lengo lake kuu ni kuunda taifa linalofanyakazi bila ya ulaji rushwa, litakalowasiadia wananchi wake na kuwa taifa huru miongoni mwa EU.

Raia wa Poland walishtushwa sana na habari za kifo cha rais wao, na mamia wakakusanyika mara moja nje ya kulu mjini Warsaw kutoa heshima zao kwa rais Kaczynski.

XS
SM
MD
LG